Mdee: Nisipotekeleza ahadi zangu sitagombea 2020


Mbunge wa Jimbo la Kawe Mh. Halima James Mdee amesema asipotekeleza ahadi alizoziadi katika kipindi cha kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka jana kwa zaidi ya asilimia hamsini hatogombea katika uchaguzi wa 2020.

Mdee aliyasema hayo jana katika kipindi cha HotMix kinachorushwa na kituo cha EATV.


“Kama sitatekeleza ahadi zangu kwa zaidi ya asilimia 50 sitagombea uchaguzi kwa kuwa kama nitashindwa kuondoa kero za wapiga kura wangu sistahili kuwa mwakilishi wao,” alisema.


Aliongeza kuwa “Lazima nilipoishia katika kipindi cha miaka mitano iliyopita nipaendeleze ili hata nikisimama mbele ya wananchi wangu kuomba kura watanipa kwa sababu sikuwaangusha.”


Alisema amefanikiwa kupunguza baadhi ya changamoto kwenye jimbo lake la Kawe ikiwemo migogoro ya ardhi, miundombinu na Maji.


“Kukijuwepo na migogoro ya ardhi kwenye Maeneo ya Kunduchi, Mabwepande, na Bunju lakini kwa sasa inapungua na wananchi wanapata hatimiliki ya ardhi,” alisema.


“Kama mbunge siyo mfuatiliaji, haziwasilishi kero za wananchi wake Mahala husika, huyo hafai,” alisema.


Alisema mbunge lazima azifahamu siasa za ndani na nje ya nchi ili aweze kuisimamia serikali ipasavyo.


Ongeza: Mdee katika uchaguzi Mkuu wa 2015 aliogombea na Kipi Warioba ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Moshi.

Na Regina Mkonde

Mdee: Nisipotekeleza ahadi zangu sitagombea 2020  Mdee: Nisipotekeleza ahadi zangu sitagombea 2020 Reviewed by on 9:25:00 PM Rating: 5

No comments: