No trouble in paradise: Zari azipuuzia tetesi zinazozidi kuvuma kuhusu kusalitiwa na Diamond


Lakini huenda tetesi hizo zikaendelea kuishia tu Instagram kwasababu wawili hao hawaoneshi dalili za kuyapoteza mahaba mazito kati yao. 
Zari alithibitisha kupitia Snapchat kuwa yeye na mpenzi wake, hitmaker wa Kidogo, Diamond wanatarajia mtoto wa pili – wa kiume, lakini tetesi za usaliti zimeendelea kuwawinda kila kukicha. 

Wikiendi hii kulisambaa picha kwenye mitandao ya kijamii inayomuonesha Hamisa Mobetto akiwa kwenye chumba cha hoteli kinachofanana kwa kiasi kikubwa na chumba ambacho Diamond alionekana akiwemo katika video aliyoiweka Instagram inayomuonesha akiuimba wimbo wake Kidogo aliowashirikisha P-Square. 

Ni katika chumba hicho pia staa huyo alikitumia akiwa na Zari. 
Picha hiyo imesababisha mjadala mkubwa wikiendi yote, huku baadhi ya mashabiki wakimshambulia Hamisa kwa kile wanachoamini anaweza kuwa sababu kubwa ya kusababisha mtafaruku katika uhusiano huo, wengine wakimuonea huruma Zari kuwa kama yasemwayo ni kweli basi hatendewi haki na mpenzi na wengine wakimshambulia Diamond kwa kuhisi anamkosea heshima mwanamke ambaye si tu amemzalia mtoto mrembo wa kike, Tiffah, bali pia yu mbioni kumbariki kwa mtoto mwingine wa kiume. 

Hata hivyo mambo yako tofauti kwa Zari ambaye post zake za Instagram na Snapchat zinatuma ujumbe mwingine – positive vibes only. Kwenye moja ya post za Snapchat, staa huyo wa Uganda anaonekana akiwa kwenye mgahawa wa kifahari huku akiionesha pete ya thamani kwenye kidole chake cha chanda.


Pia kwenye Instagram amepost picha na kupeleka ujumbe huo huo – no trouble in paradise. 




No trouble in paradise: Zari azipuuzia tetesi zinazozidi kuvuma kuhusu kusalitiwa na Diamond No trouble in paradise: Zari azipuuzia tetesi zinazozidi kuvuma kuhusu kusalitiwa na Diamond Reviewed by on 3:59:00 AM Rating: 5

No comments: