Mwanamuziki wa Bongo Flava anayesimamiwa na Wasafi, Harmonize,
amekanusha kuchunwa pesa na mpenzi wake Jackline Wolper kutokana na
mwanamke huyo kuonekana kuwa na maisha ya kifahari.
Harmonize amekanusha hayo kwa kusema
“Nyumbani kwa Wolper kuna kaunta ambayo anaweza kunywa vinywaji
atakavyo, pia sioni sababu ya mimi kupendeza na mwanamke wangu
asipendeleze ni lazima nitahakikisha anapendeza kwa kuwa ninampenda”.
Harmonize pia alizidi kuweka wazi kuwa mapenzi yake na Wolper
hajaathiri kitu chochote kwenye kusaidia familia ya kwao kwa kuwa hata
kama asingekuwa na Wolper ni lazima angekuwa kwenye mahusiano.
“Siyo kwamba ninatumia pesa nyingi kumridhisha mpenzi wangu na
kusahau familia yangu, Mama yangu na ndugu zangu wanapata pesa za
matumizi kama kawaida kwa kuwa ninafanya kazi”.alisema Hrmonize.
Harmonize Akanusha Kuchunwa Pesa na Jack Wolper
Reviewed by
on
8:55:00 AM
Rating:
No comments: