Ofisa Ardhi na Mipango Miji wa Wilaya ya Ilala, Paul Mbembela na Ofisa Mipango Miji Wilaya ya Kinondoni, Juliana Letara ndiyo watumishi ambayo Makonda anadai kuwa wameshindwa kutoa taarifa za mipango miji katika maeneo wanayoyasimamia na kuorodhesha maeneo ya wazi yaliyovamiwa.
Amezungumza hayo jana jijini Dar es Salaam, wakati alipofanya mkutano na madiwani na watendaji wa mkoa huo, uliokuwa na lengo la kujadili suluhisho la uvamizi wa maeneo ya wazi.
“Ili kunisaidia mimi kuchukua hatua ya kurejesha maeneo hayo nina wapa siku 10 madiwani wote mkoa wa Dar kuhakikisha wanarejesha ripoti za maeneo yao ili yatumike kwa matumizi yaliyokusudiwa,” alisema.
“Watumishi hawa watambue kuwa sheria itafuata mkondo wake ikiwa ni pamoja na kuwasimamisha kazi pamoja na kuwawajibisha kwa kufuata sheria. Hatuwezi kuendelea kupoteza maeneo haya kwa sababu ya kushindwa kusimamia, ni lazima kila aliyehusika kusababisha upotevu huu awajibishwe,” aliongeza.
“Jiji la Dar es Salaam lina changamoto nyingi za uvamizi wa viwanja vya wazi na kwamba jambo la kushangaza wavamizi hao, wanazo hati miliki huku pia wamiliki halali wakiwa na hati. Maeneo ya viwanja vya mpira yamevamiwa, maeneo ya shule yamevamiwa, maeneo ya zahanati yamevamiwa, lakini wavamizi wote wana hati miliki. Jambo la kujiuliza wamezitoa wapi? Nani aliyehusika kuwauzia? Ni wajibu wenu kuyapitia na kuyabainisha maeneo yote.”
Alisema ofisi yake itachukua hatua kali kwa watumishi waliohusika kuuza au kubadilisha ramani ya viwanja vya wazi na kusababisha viwanja hivyo kupotea. Pia amewataka wananchi waliovamia maeneo ya wazi ambayo yametengwa kwa matumizi mbalimbali kama ujenzi wa shule, zahanati na masoko, kubomoa nyumba zao kwa gharama zao kabla ya hatua kali hazijachukuliwa dhidi yao.
Makonda apendekeza kutumbuliwa kwa maafisa hawa Dar
Reviewed by
on
6:43:00 AM
Rating:
No comments: