KESI ya shambulio inayowakabili Halima Mdee, Mbunge wa Kawe; Saed
Kubenea, Mbunge wa Ubungo na Mwita Waitara, Mbunge wa Ukonga
imeahirishwa leo katika Mahakama ya Kisutu kutokana na upande wa
mashtaka kutokamilisha upelelezi.
Washitakiwa wengine kwenye kesi hiyo ni Shafii Juma, mfuasi
wa Chadema; Manase Mjema, Diwani wa Kimanga pamoja na Alfonce Kinyafu,
Diwani wa Kimara Saranga ambao kwa pamoja wanadaiwa kumshambulia
Theresia Mmbando, Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam wakati wa harakati
za Uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es Salaam.
Helleni Liwa, Hakimu Mkazi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ameahirisha kesi hiyo mpaka tarehe 2 Juni mwaka huu.
Kesi na Mdee,Kubenea yapigwa kalenda
Reviewed by
on
10:44:00 PM
Rating:
No comments: